• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kumbukumbu ya ushirikiano iliyosainiwa na China na WHO kuhusu sekta ya afya itasaidia jamii ya kimataifa kupambana na matishio ya kiafya

    (GMT+08:00) 2017-01-19 19:03:29

    Aliyekuwa msaidizi wa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Liu Peilong amesema afya ni sehemu muhimu kwenye pendekezo linalotetewa na China la "jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja", hivyo jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua kwa pamoja ili kupambana na matishio ya kiafya yanayoikabili dunia.

    Bw. Liu amesema hayo baada ya China na WHO leo mjini Geneva kusaini kumbukumbu ya ushirikiano wa sekta ya afya kwenye "Ukanda Mmoja na Njia Moja", hafla iliyoshuhudiwa na rais Xi Jinping wa China na mkurugenzi mkuu wa WHO Margaret Chan.

    Kumbukumbu hiyo inaonesha kuwa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja hakuwezi kuachana na jumuiya yenye hatma ya pamoja ya afya na usalama wa watu, hivyo nchi, mashirika ya kimataifa na jamii za kiraia zinapaswa kushirikiana katika kukabiliana na matishio ya kiafya duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako