• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea nchini Mali

    (GMT+08:00) 2017-01-19 20:55:50

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Baraza la Usalama la Umoja huo wametoa taarifa wakilaani shambulizi la kujitoa mhanga kwa kutumia gari lililotokea mjini Gao, Mali ambalo kundi la kigaidi la Nasserism Independent Movement limetangaza kulifanya.

    Taarifa zimetolewa baada ya gari moja lililotegwa mabomu kulipuka kwenye kambi moja ya jeshi mjini Gao hapo jana, na kusababisha vifo vya watu 50 na wengine 60 kujeruhiwa. Katibu mkuu ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na serikali ya Mali, na kutaka washukiwa wa shambulizi hilo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

    Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametoa salamu za pole kwa serikali ya Mali na familia za wafiwa, na kusema ugaidi wa aina yoyote ni moja ya tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako