• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi apongeza mafanikio ya shughuli za Mwaka wa utamaduni wa China na Misri

    (GMT+08:00) 2017-01-20 09:55:06

    Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwenye ufungaji wa Shughuli za Mwaka wa Utamaduni kati ya China na Misri uliofanyika jana mjini Guangzhou.

    Kwenye salamu zake rais Xi amesema, mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka wa 60 tangu China na Misri zianzishe uhusiano wa kibalozi. Katika kipindi hicho, kutokana na juhudi za pamoja, uhusiano kati ya China na Misri umeendelea kukua na kuwa mfano wa kuigwa kwa mahusiano ya Kusini na Kusini.

    Rais Xi amesisitiza kuwa hii ni mara ya kwanza kwa China kufanya shughuli za mwaka wa utamaduni na nchi ya kiarabu, ikiwa ni hatua muhimu ya nchi hizo mbili za kuimarisha maelewano kati ya watu wao chini ya Pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja. Ameongeza kuwa China inapenda kuendelea kuhimiza ushirikiano wa kiutamaduni na Misri ili kuimarisha msingi wa umma kwa maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako