• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vivian Cheruiyot awa mwanaspoti bora nchini Kenya mwaka 2016

    (GMT+08:00) 2017-01-20 09:59:04

    Mshindi wa medali ya dhahabu ya mbio za mita 5,000 na medali ya fedha ya mbio za mita 10,000 za Olimpiki, Vivian Cheruiyot ndiye mwanaspoti bora nchini Kenya mwaka 2016. Cheruiyot, ambaye amejishindia Sh milioni 1 za Kenya, alishinda taji hili mwaka 2011. Katika tuzo ya mwaka 2016, amembwaga bingwa wa marathon za London na Olimpiki, Eliud Kipchoge na wachezaji walemavu Samuel Muchai na Nancy Koech.

    Mkimbiaji huyu anayefahamika kwa jina la utani kama Pocket Rocket, aliweka rekodi mpya ya Olimpiki katika mbio za mita 5,000 kwa dakika 14:26.17 jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. Aliongoza Mkenya mwenzake Hellen Obiri kunyakua nafasi mbili za kwanza wakimduwaza Almaz Ayana wa Ethiopia. Cheruiyot alinyakua nishani ya fedha ya mbio za mita 10, 000 jijini Rio katika rekodi mpya ya dakika 29:32.53 akimaliza nyuma ya Ayana, ambaye aliweka rekodi ya dunia ya 29:17.45.

    Ni tuzo ya pili ya Cheruiyot mwaka 2016 baada ya kushinda zawadi ya mwanaspoti bora wa kike wa mwaka katika tuzo za Shirikisho la Riadha la Kenya (AK), ambapo aliwalemea mabingwa wa Olimpiki Faith Chepng'etich mita 1,500 na Jemimah Sumgong mbio za marathon. Cheruiyot ni mwanaspoti wa tatu kushinda tuzo hii baada ya Catherine Ndereba na Janeth Jepkosgei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako