Bw Wabukala atachukua nafasi ya Bw. Philip Kinisu anayelazimika kujiuzulu kutokana na familia yake kutuhumiwa kupokea dola milioni 7.91 za kimarekani kutoka kwa Shirika la kitaifa la huduma kwa vijana NYS.
Taarifa ya bunge la Kenya imesema Rais Kenyatta amemtakia Bw. Wabukala kuwa na mafaniko kwenye wadhifa mpya, akisisitiza kuwa Bw. Wabukala ni kiongozi anayeaminika na kuheshimika, na ana uwezo wa kuongoza vizuri tume ya kupambana na rushwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |