• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Adama Barrow aapishwa kuwa rais mpya wa Gambia nchini Senegal

    (GMT+08:00) 2017-01-20 10:45:49

    Bw. Adama Barrow ameapishwa kuwa rais wa Gambia kwenye ubalozi wa nchi hiyo mjini Dakar, Senegal. Akihutubia muda mfupi baada ya kuapishwa Bw Barrow aliwashukuru waungaji mkono wake ambao kwa mara ya kwanza wamechagua rais kwa kupiga kura, na kusema atarudi Gambia haraka iwezekanavyo na kuunda serikali.

    Bw. Barrow alichaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 2 Desemba mwaka jana, lakini hawezi kuchukua madaraka moja kwa moja kutokana na upinzani wa rais wa zamani Yahya Jammah.

    Umoja wa Ulaya umemtaka rais Jammeh aheshimu matokeo ya uchaguzi na kukabidhi madaraka kwa Bw. Barrow. Umoja wa Mataifa umezitaka pande mbalimbali za Gambia na nchi nyingine za Afrika Magharibi kuhakikisha amani katika kipindi cha makabidhiano ya madaraka nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako