• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wakulima wa Kenya wapigwa jeki baada ya shirika la ndege la KQ kusaini mkataba wa kusafirisha maua Australia

    (GMT+08:00) 2017-01-20 19:17:18

    Wakulima wa maua wamepigwa jeki baada ya shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) kukubali kusafirisha tani 30 za maua nchini Australia.

    Meneja wa mizigo na mauzo wa shirika hilo Bi Patricia Odida amesema huduma hiyo mpya ya KQ ,kwa ushirikiano na shirika la ndege la Australia la Qantas Airways,itasaidia wakulima wa maua na mboga Kenya kusafirisha bidhaa zao Australia na nchi zinazopakana nayo.

    Odida amesema kupitia ushirikiano huo,wameanzisha huduma thabiti ya usambazaji ambayo imesaidia kuanzisha upya hitaji la maua ya Kenya nchini Australia.

    Aidha Odida amesema ushirikiano huo unafungua soko la Australia kwa wasafirishaji na pia ni fursa ya biashara kwao ya kuongeza mapato.

    Mwka 2015 Kenya iliuza jumla ya tani 122,000 za maua zenye thamani ya Sh63 bilioni kwa Umoja wa Ulaya,kutoka tani 114,000 mwaka 2014.

    Mwaka jana uzalishaji ulipungua kidogo kutokana na hali mbaya ya hewa lakini kulipatikana marejesho mazuri ya zaidi ya Sh10 bilioni.

    Kenya ina mashamba 127 ya maua na nusu ya mashamba hayo yanapatikana karibu na ziwa Naivasha na mengine yanapatikana kaunti za Nyeri,Kiambu,Embu,Kirinyaga,Nakuru,Uasin Gishu,Baringo,Trans Nzoia na Narok.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako