• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Morogoro:Wananchi wapigwa marufuku kuuza chakula

    (GMT+08:00) 2017-01-20 19:17:32

    Serikali ya Tanzania imepiga marufuku wananchi wa Morogoro kuuza chakula .

    Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Stephen Kebwe wakati alipokuwa akizungumzia hali ya chakula mkoani humo,na kusema kuwa hivi sasa kuna upungufu wa chakula,na si ruhusa kwa yeyote kuuza chakula alicho nacho.

    Aliongeza kuwa imebidi atoe tahadhari hiyo kwa sababu wananchi wengine wanatumia vibaya chakula walicho nacho kwa kupika pombe halafu wakisubiri serikali iwaletee chakula cha msaada.

    Aidha Mkuu huyo wa mkoa alisema ni vyema kwa wananchi kujiwekea akiba ya kutisha ya chakula ili kuepuka upungufu wa chakula,na pia wakulima kupanda mazao yanohimili ukame.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako