• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Waganda waishio ughaibuni washauriwa kuwekeza nyumbani

    (GMT+08:00) 2017-01-20 19:17:56

    Naibu Mwenyekiti wa Uganda Convention nchini Uingereza amewashauri waganda waishio ughaibuni kuwekeza nyumbani kutokana na hali nzuri ya uwekezaji iliyowekwa na serikali.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama cha Uganda Convention nchini Uingereza ,Bernard Robinson Magulu ambaye pia ni mwakilishi wa chama hicho nchini Uganda,amesema serikali ya Uganda kupitia kwa mashirika mbalimbali imeweka mikakati bora ya kurahisisha uwekezaji nchini humo.

    Magulu amesema Mamlaka ya Uwekezaji nchini Uganda (UIA) inaanzisha maeneo ya kiviwanda na biashara nchini kote ambayo yanalenga kutangaza teknolojia mpya za utafiti na kuongeza uzalishaji wa mapato nchini humo.

    Magulu amewashinikiza waganda waishio ughaibuni kuanzisha biashara zinazolenga viwanda katika sehemu wanazotoka.

    Uganda Convention ni kongamano la waganda kutoka sehemu mbalimbali za dunia jijini London,Uingereza.

    Kongamano hilo huwaleta pamoja wataalamu,viongozi wa biashara,wawakilishi wa mashirika mbalimbali kutoka Uganda,Uingereza na Kimataifa.

    Kongamano la mwaka huu litaandaliwa tarehe 16 Septemba ,Troxy,jijini chini ya kaulimbiu "kushirikiana kwa ajili ya kujenga utajiri".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako