Takwimu rasmi zilizotolewa leo na Idara ya Takwimu ya Taifa ya China zinaonesha kuwa mwaka jana uchumi wa China ulikua kwa asilimia 6.7, ikiwa ni kasi ndogo zaidi ya ongezeko katika miaka 26 iliyopita, lakini inaendana na lengo lililowekwa na serikali.
Kwa mujibu wa Idara hiyo, pato la taifa la China lilifikia dola za kimarekani trilioni 10.83, huku sekta ya huduma ikichukua asilimia 51.6.
Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa viashiria vikuu vya kiuchumi vililegea mwaka jana, ambapo ongezeko la uzalishaji wa kiviwanda lilipungua hadi kwa asilimia 6 kutoka asilimia 6.1 ya mwaka 2015.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |