Wizara ya mambo ya nje ya China imepuuza hatua ya Taiwan kupeleka ujumbe wake kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Donald Trump, na kusema hatua hiyo inalenga kuvuruga uhusiano kati ya China na Marekani.
Msemaji wa wizara hiyo Hua Chunying amesema, serikali ya Marekani imethibitisha kuwa itaalika mabalozi wa nchi za nje walioko nchini Marekani kuhuduria hafla hiyo, na haipendekezi nchi au sehemu nyingine kupeleka wawakilishi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |