• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi ya Uingereza (EPL) imeendelea jana Arsenal yashinda

    (GMT+08:00) 2017-01-23 09:16:54

    Arsenal wakiwa kwao Emirates wamefanikiwa kushinda 2-1 kwa penalty dakika za majeruhi wakati wakiwa wachezaji 10 tu uwanjani baada ya kiungo wao Xhaka kulimwa kadi nyekundu, na baadae kocha wao Arsene Wenger kutolewa je ya uwanja.

    Arsenal walianza kufunga dakika ya 59 kwa bao la Sentahafu wao Mustafi. Burney walisawazisha kwa penalty iliyofungwa na Andrey Gray dakika ya 93 baada ya Francis Coquelin wa Burney kumchezea faulo Ashley Barnes.

    Dakika ya 98 Refa aliwapa Arsenal penalty baada ya buti la Ben Mee kuwa kichwani mwa Laurent Koscienly na Alexis Sanches kuwafungia Aresal bao la pili na la ushindi.

    Mechi nyingine, Southampton wakiwa kwao Saint Mary, waliwatandika mabingwa watetezi Leicester City 3-0 kwa magoli ya Ward Prowse, Rodriguez na penalty ya Tadic.

    Chelsea imeisambaratisha Hull City 2-0. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Diego Costa "Mnyama" dakika ya 45 na Cahill alifunga kwenye dakika ya 81 na kuifanya Chelsea kuendelea kuongoza ligi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako