• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa yuan bilioni 91.78 ili kuhakikisha maisha ya watu maskini wakati wa majira ya baridi na mchipuko

    (GMT+08:00) 2017-01-23 18:17:27

    Habari kutoka ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China zinasema, China imetenga yuan bilioni 91,78 ili kuhakikisha maisha ya watu maskini wakati wa majira ya baridi na mchipuko. Asilimia ya 80 ya fedha hizo zimesambazwa kwa watu husika, na nyingine zitaendelea kusambazwa kwa watu waliokumbwa na maafa.

    Wizara ya mambo ya ndani ya China imefanya tathmini kuhusu watu wanaohitaji msaada, na kuthibitisha kuwa kuanzia majira ya baridi ya mwaka jana hadi majira ya mchipuko ya mwaka huu, watu milioni 51.97 watahitaji msaada wa chakula, na watu milioni 17.11 watahitaji msaada wa nguo na mablanketi.

    Naibu waziri wa mambo ya ndani wa China Bw. Gong Puguang amesema wizara ya mambo ya ndani ya China itazihimiza serikali za mitaa zitekeleze kwa makini sera na hatua mbalimbali za kuwasaidia watu maskini, na kuharakisha mchakato wa kusambaza fedha, ili kuhakikisha watu wanaohitaji msaada wanapata pesa hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako