• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la kimataifa latwaa udhibiti wa Ikulu ya Gambia

    (GMT+08:00) 2017-01-23 18:30:14

    Jeshi la jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi limetwaa udhibiti wa Ikulu ya Gambia siku moja baada ya kuondoka kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Bw Yahya Jammeh.

    Habari zinasema jeshi hilo lilikumbana na vizuizi kiasi kutokana na walinzi wa Ikulu kuweka vizuizi. Ofisa mmoja wa jeshi kutoka Senegal alisema mkuu wao alikuwa anafanya mazungumzo na walinzi wa Ikulu. Kutokana na kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Ikulu hakuonekana, jeshi la kimataifa lililazimika kufanya mazungumzo ya muda mrefu na kaimu mkuu, kabla ya kuruhusiwa kuingia ndani.

    Bw Jammeh alitangaza kwa njia ya televisheni kuachia madaraka na kuondoka mjini Banjul, na kuruhusu Rais mteule Bw Adama Barrow kurudi mjini Banjul kutoka Dakar, Senegal na kuchukua madaraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako