• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Nchi 50 zaunga mkono Amina Mohamed kuwa mwenyekiti wa AU

    (GMT+08:00) 2017-01-24 19:58:42

    Juhudi za Waziri wa mashauri ya nchi za Kigeni Amina Mohamed kuwania uwenyekiti wa muungano wa Afrika zinaendelea kuzaa matunda kwani sasa nchi tofauti zimekubali sera zake.

    Mataifa 50 barani Afrika yameunga mkono uwaniaji wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Amina Mohammed kwa wadhifa wa mwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika.

    Waziri wa elimu Dr. Fred Matiang'i ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya baraza la mawaziri inayoshughulikia suala la uungwaji mkono wa Mohammed kwa wadhifa huo alisema Kenya itakamilisha kampeni yake kwa kuandaa kikao na wajumbe maalum kutoka Benin na Guinea Bissau juma hili ili kuwashawishi kumuunga mkono waziri huyo.

    Mohammed tayari ameondoka hapa nchini Kenya kuelekea nchini Benin kabla ya kuhudhuria kikao kuhusu masuala ya jinsia nchini Ethiopia. Uchaguzi huo unatarajiwa kujaza nafasi zote 10 za tume hiyo ikiwemo ile ya naibu mwenyekiti na nane za makamishna.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako