Taarifa iliyotolewa jana na AMISOM imesema jeshi la pamoja limewashambulia vikali wapiganaji wa Al-Shabaab katika operesheni hiyo iliyofanywa mapema jana, ambapo wapiganaji hao walijaribu kujibu mashambulizi ili kuteka tena mji wa Badade.
Badade ni mji muhimu wa pwani katika eneo la Lower Juba, kusini mwa Somalia, ambao ulidhibitiwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab baada ya vikosi vya Kenya kuondoka mwezi Januari mwaka jana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |