• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya ina matumaini Amina Mohamed atakuwa mwenyekiti mpya wa AU

    (GMT+08:00) 2017-01-25 12:46:21

    Kenya ina matumaini kwamba waziri wake wa mambo ya kigeni Amina Mohamed atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika kwenye uchaguzi ujao.

    Serikali imekuwa ikitafuta kuungwa mkono na nchi mbalimbali za kikanda na kote barani humo ili kumuunga mkono Amina kupata nafasi hiyo ya juu zaidi kwenye Umoja wa Afrika wenye nchi 54.

    Wiki hii serikali inakamilisha hatua za mwisho za kabla ya uchaguzi wa wiki ijayo Ronald Mutie anaripoti kutoka Nairobi.

    Ni matumaini ya dakika za mwisho ya Kenya, kwamba waziri wake wa mambo ya kigeni Amina Mohamed ataibuka mshindi na kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

    Imesalia siku sita kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo wakati wa mkutano wa 28 wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia.

    Serikali ya Kenya hadi sasa imefanya kampeni ya kutafuta uungwaji mkono katika nchi 51 za Afrika.

    Na niki hii mawaziri mbalimbali wakiongozwa na mke wa Rais Magaret Kenyatta

    Fred Matiang'i waziri wa elimu ni mmoja wa wanachama wa kamati maalum inayoongoza kampeni za kuhakikisha Amina Mohamed anachaguliwa.

    "Mwaniaji wetu ambaye ni waziri, Amina amekuwa kwenye msitari wa mbele akifanya kazi na vijana, makundi ya wanawake na kuhakikisha anaunganisha kila mtu kwa manufaa ya bara lote la Afrika. Yeye ni mwenye uzoefu mkubwa na anaheshika kote barani Afrika"

    Amina Mohamed kabla ya kuwa waziri wa mambo ya kigeni, alihudumu kama naibu mkurungezi wa shirika la umoja wa Mataifa la kuhifadhi mazingira UNEP.

    Anategemea uzoefu wake wa kidiplomasia na kazi aloiyofanya kwenye ngazi ya kimataifa kuibuka na ushindi, anasema.

    "Tungependa kutumia fursa hiyo kujinufaisha kiuchumi kuhakikisha kwamba hadhi yetu inasalia imara na pia ni ishara ya kujitolea kwetu kutumikia bara letu. Naweza kuwambia kwamba tumefanya kazi kwa bidii na rais ametia juhudi kubwa kwenye kampeni hii na angependa kuona nafasi hii inachukuliwa na Kenya"

    Iwapo atashinda, Amina Mohamed akiwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika atakuwa na jukumu la kutekelezwa kwa agenda ya Umoja huo ya mwaka 2063, kutafuta mikataba bora ya kibiashara na kuratibu amani na usalama.

    Lakini Amina pia anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wawaniaji wengine watano wakiwemo mawaziri wa mambo ya kigeni wa Botswana Pelonomi Venson-Moitoi, Moussa Faki Mahamat wa Chad, Agapito Mba Mokuy wa Equatorial Guinea na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati Bathily Abdoulaye kutoka Senegal.

    Kulingana na mchambuzi wa maswala ya kisiasa Barrack Muluka, ushindi wa Amina Mohamed hauwezi kuhakikishwa na uchaguzi huo kuenda ukaingia kwenye awamu ya pili.

    "Haya mambo ya kidiplomasia hutegemea maslahi ya kila nchi. Itategemea pia na zile nchi zingine kwa sababu kuna watu wengine amabo pia wanataka. Nitampa. 50-50 lakini sifikirii kuwa ni kitu kitashinda katika awamu moja"

    Kwa sasa wadhifa huo wa wenyekiti wa Tume ya Afrika unashikiliwa na bibi Dlamini Zuma na naibu wake akiwa ni Erastus Mwencha.

    Dlamini-Zuma ambaye amekuwa mwenyekiti wa AU tangu mwaka wa 2012 hajaomba tena nafasi ya kuwania kwa muhula wa pili.

    Uchaguzi wa wiki ijyao pia utajumuisha kuchaguliwa kwa naibu wa mwenyekiti na makamishena wanane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako