• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa kuunga mkono makabidhiano ya madaraka kwa amani nchini Gambia

    (GMT+08:00) 2017-01-26 12:50:42

    Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika kanda ya Afrika magharibi Bw. Mohamed Ibn Chambas ameliarifu Baraza la usalama la umoja huo kuwa Umoja wa Mataifa utaunga mkono utulivu na ujenzi wa Gambia.

    Bw. Chambas amesema ataendelea na juhudi za kuhimiza makabidhiano ya madaraka kwa amani na kutoa wito wa mshikamano na maafikiano ya kitaifa nchini humo.

    Mkutano huo ni mwendelezo wa Azimio nambari 2237 lililopitishwa Januari 19 na Baraza la usalama kuhusu msukosuko wa Gambia, ambalo linamtaka katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kutoa ripoti kwa baraza hilo ndani ya siku kumi.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, rais Adama Barrow wa Gambia aliyeapishwa katika ubalozi wa nchi hiyo nchini Senegal anatarajiwa kurudi leo nchini Gambia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako