• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa misaada ya vifaa vya matibabu kwa hospitali ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-01-27 10:56:37

    Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini umesema serikali ya China imetoa msaada wa dawa na vifaa vya matibabu vyenye thamani ya doal elfu 60 za kimarekani kwa Hospitali ya Urafiki ya Paloich iliyoko katika jimbo la Upper Nile, kaskazini mwa Sudan Kusini.

    Msaada huo ni pamoja na aina 27 za dawa na aina 9 za vifaa vya matibabu.

    Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw He Xiangdong amesema ushirikiano wa kiutendaji kati ya China na Sudan Kusini kwenye sekta ya afya umepata mafanikio katika miaka ya karibuni. Kikundi cha madaktari wa China nchini Sudan Kusini, na udhamini wa mafunzo ya udaktari unaotolewa na China vimehimiza maendeleo ya hudumu za afya nchini Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako