• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump asaini mpango wa kuchunguza wakimbizi

    (GMT+08:00) 2017-01-28 19:19:54

    Rais wa Marekani Donald Trump amesaini mpango juu ya kusimamia wakimbizi wanaoingia nchini Marekani kwa jina la kujilinda dhidi ya vitisho vya ugaidi.

    Ikulu ya Marekani ilitoa waraka usio na maelezo lakini vyombo vya habari vimependekeza kuwa inawezekana sheria hiyo ni kuwazuia wakimbizi toka Syria kwa muda usiojulikana, na kwa miezi minne ya kuzuia wakimbizi wengine ikiwa ni hatua ya serikali ya Marekani kutathmini kiwango cha hatari kwa kila nchi.

    Ripoti hiyo pia imependekeza Marekani kujiepusha kutoa vibali kwa wananchi wa Iran, Sudan, Syria, Libya, Somalia, Yemen na Iraq nchi ambazo inadaiwa Serikali zao zimo katika orodha ya Marekani ya kuwa wafadhili wa vikundi vya ugaidi au kukumbwa na wasiwasi.

    Hatua hii mpya ya rais Trump, si sawa na ya kupiga marufuku waislamu aliyoipendekeza wakati wa kampeni za kugombea urais. Pia Trump amesaini mpango wa kuimarisha jeshi la Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako