• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wapongeza China kwa kuchangia amani na maendeleo ya dunia

    (GMT+08:00) 2017-01-28 19:21:53

    Mwenyekiti wa kikao cha 71 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Peter Thomson amesema China itachangia amani na maendeleo ya dunia kwa kutoa ahadi za kuunga mkono utandawazi na sera ya pande nyingi.

    Bw. Thomson amesema wazo linalotetewa na China la kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja ni mustakbali pekee wa binadamu kwenye sayari hii ya dunia, na kwamba binadamu wanapaswa kuwa na mfumo unaojengwa kwa kanuni fulani na kupata maendeleo kwa njia za kiustaarabu. Ameeleza imani yake kuwa China itashirikiana na jamii ya kimataifa, kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu na makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na kutoa mchango kwa vizazi vijavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako