• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika washutumu mashambulizi kwenye kituo cha AMISOM

    (GMT+08:00) 2017-01-30 18:05:51

    Umoja wa Afrika umelaani mashambulizi yaliotekelezwa na kundi la wapiganaji wa al-shabaab katika kituo cha walinda amani wa umoja huo nchini Somalia eneo la Kolbiyow.

    Serah Nyakaru yuko mjini Addis Ababa Ethiopia ambako mkutano wa 28 wa Umoja wa Afrika unafanyika na ametuandalia ripoti ifuatayo.

    Naibu Mwenyekiti wa Kamishena wa Tume ya Umoja wa Afrika Erastus Mwencha ameshutumu mashambulizi katika kituo cha AMISOM mjini Kolbiyow, na wanamgambo wa Al Shabaab.

    "Kwanza tunataka kusimama na nchi na familia wakati huu lakini pia tunapaswa kuangalia jinsi gani tunaweza maliza mashambulizi haya, katika siku za nyuma tumefanya bidii ili kupunguza mashambulizi"

    Mwanche amesema mashambulizi haya hayathiri waliopoteza jamaa zao, bali bara la Afrika kwa jumla.

    "Ni wasiwasi kwetu kwa sababu tukipoteza mtu mmoja bara la Afrika ndilo linamwaga damu, na tukufikiri msaada wanachama wetu wamepa vijana ambao wamechukua njia ya silaha kuweza kutulinda, ni huzuni sana wakati wanapoteza maisha yao kwa njia hii, ni uchungu sana, na tukifiria vile vijana wamejitolea kuenda uko nje kutulinda, wakipoteza maisha kwa njia hii ni uchungu sana"

    Jeshi la Kenya walithibitisha kuwa tisa ya wafanyakazi wake waliuawa na wengine 15 walijeruhiwa katika shambulizi la wanamgambo wa Al Shabaab.

    Msemaji wa (KDF) Kanali Paul Njuguna amesema wanamgambo zaidi ya 70 wa Al-Shabaab waliuawa na na vikosi vya askari ambao wanafanya kazi chini ya muungano wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

    Kwa mujibu wa Mwencha, Umoja wa Afrika AU imelaani kitendo hicho kwa kuonyesha umoja wake kwa serikali ya Kenya na waathiriwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako