• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dlamini Zuma atoa hotuba yake ya mwisho

    (GMT+08:00) 2017-01-31 20:00:00

    Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake ofisini, Dr Nkosazana Dlamini Zuma alitoa hotuba yake ya mwisho, katika kikao 28 cha wakuu wa nchi na serikali ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia.

    Mwanahabari wetu Serah Nyakaru yuko mjini Addis Ababa Ethiopia ambako mkutano wa 28 wa Umoja wa Afrika unafanyika na ametuandalia ripoti ifuatayo.

    Dr Nkosazana Dlamini Zuma, ameaza hotuba yake kwa kumkaribisha katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na baadaye kumpongeza Amina J Mohamed kutoka Nigeria kwa kuchanguliwa kama Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

    Sauti ; Nkosazana Dlamini Zuma

    "kwanza nataka kumkaribisha katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia nataka jinsi tumefurahia uchanguzi wa bi Amina J Mohamed kama Naibu katibu mkuu"

    ikiwa hii ndio hotuba yake ya mwisho kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, ameomba watu kuthamini vijana, kwa sababu bara la Afrika liko wanawake na vijana milioni 200 kati ya miaka 15 na 24.

    Sauti ; Nkosazana Dlamini Zuma

    "tukianza huu mwaka wa vijana lazima tujitolea kuthamini vijana wetu, bara la Afrika liko na vijana na wanawake milioni 200 kati ya miaka15 na 24, na ifikapo mwaka wa 2025 robo ya duniani itakuwa ni vijana"

    bi zuma anataja baadhi ya mambo ambayo yanafanya mwaka huu kuwa mwaka mzuri.

    Sauti ; Nkosazana Dlamini Zuma

    "Mwaka wa 2017 unafikisha miaka 55 tangu kuanzishwa kwa shirika la utetezi wa wanawake katika nchi za Afrika mwaka wa 1962 kabla ya shirika la umoja wa Afrika"

    Anaendelea kusema kazi ya PAWO hii leo ni kung'ang'ana katika kuwezesha watoto wakike na wanawake, kupitia masomo na ujuzi, katika nyanja za kisiasa, jamii, utamaduni na kiuchumi.

    Sauti ; Nkosazana Dlamini Zuma

    "kazi ya PAWO hii leo kuendelea kupambana katika kuwezesha watoto wakike na wanawake kupitia elimu na ujuzi, nyanja za kisiasa,kijamii, kitamaduni na kiuchumi. ni lazima waendelee kutete na kufanyakazi kwa ajili ya amani Afrika na salama kwa watu wote"

    Alitumia wakati huu kumshukuru mwenyekiti wa umoja wa afrika aliyemaliza muda wakati.

    Sauti ; Nkosazana Dlamini Zuma

    "wacha nichukuwe fursa hii, kumshukuru mwenyekiti wa umoja wa afrika aliyemaliza muda wake, rais mheshimiwa wa demokrasia ya Chad Idriss Ito Deby, kwa uongozi wake ofisini, na vile endesha mambo muungano wakati mwaka wake ofisini"

    Mkurungenzi mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amempongeza mwenyekiti mwenda zake wa tume ya umoja wa afrika Dr Nkosazana Dlamini Zuma na msaidizi wake kwa kazi njema walioifanya wakati walipokuwa ofisini.

    sauti ;Bw Antonio Guterres

    "Na mpongeza mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Dr Nkosazana Dlamini Zuma , naibu Erastus Mwencha na makamishina AU kwa juhudi zao za kukuza mageuzi ya kijamii na kiuchumi Afrika, namatakia bi zuma maisha mazuri katika siku za baadaye"

    Bw Antonio Guterres ameahaidi kufanyakazi na Umoja wa Afrika.

    "Tutafanya kazi pamoja na nyinyi wakati wowote migogoro au tishio la mgogoro linatishia utulivu na ustawi wa watu"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako