• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzalishaji nchini China waonyesha ishara za kutuliza uchumi

    (GMT+08:00) 2017-02-01 18:37:34

    Sekta ya utengenezaji nchini China imeendelea kupanuka katika kipindi cha miezi sita mfululizo, ikiwa ni ishara kuwa uchumi unatulia licha ya matarajio yasio na uhakika ya uchumi wa dunia.

    Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Takwimu ya China zimeonyesha kuwa, viashiria vya manunuzi katika sekta ya utengenezaji vimefikia alama 51.3 mwezi Januari, ikiwa ni chini kwa alama 0.1 mwezi Disemba mwaka jana.

    Pato la ndani la China GDP limekuwa kwa asilimia 6.7 mwaka jana, ikiwa ni la chini zaidi katika miaka ya karibuni, lakini ikiwa sawa na malengo yaliyowekwa na serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako