• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aeleza wasiwasi kuhusu kuvunjika kwa utaratibu wa kuwalinda wakimbizi duniani

    (GMT+08:00) 2017-02-01 18:39:30

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres ametoa taarifa juu ya suala la wakimbizi, na kueleza wasiwasi wake kuhusu kuvunjika kwa utaratibu wa kuwalinda wakimbizi duniani.

    Bw. Guterres amesema, nchi mbalimbali zina haki na wajibu wa kulinda mipaka yao dhidi ya makundi ya kigaidi, lakini udhibiti huo haupaswi kutekekelezwa juu ya misingi ya ubaguzi wa kidini, kabila au utaifa, na ni kinyume na maadili ya kimsingi ya jamii ya binadamu, ambayo inaweza kurahisisha propaganda za makundi ya kigaidi. Kwa mujibu wa msemaji wa katibu mkuu huyo Stephane Dujarric, taarifa hiyo inaeleza msimamo wa Guterres wa kupinga sera mpya za Marekani zinazohusu wahamiaji na wakimbizi.

    Wakati huohuo, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema, karibu wakimbizi 26,000 wa Somalia waliokimbilia nchini Kenya kukimbia mapigano nchini mwao na waliopanga kuweka makazi mapya nchini Marekani, wamekwama kutokana na marufuku iliyowekwa na serikali ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako