• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zapaswa kuondoa mashindano

    (GMT+08:00) 2017-02-02 19:14:05

    Balozi wa China nchini Marekani Cui Tiankai amesema, China na Marekani zinatakiwa kuacha mashindano yanayoharibiana na badala yake, kutilia maanani masuala yanayonufaisha ushirikiano kati yao.

    Akishiriki kwenye sherehe ya mwaka mpya wa kijadi wa kichina katika ubalozi wa China nchini Marekani, Bw. Cui amesema, kanuni ya uhusiano kati ya China na Marekani ni kutopambana, kutoharibiana, kuheshimiana na kunufaishana. Pia amesema, mawasiliano ya kiutamaduni yatasaidia kuongeza maelewano kati yao.

    Habari zinasema, Bw. Terry Branstad aliyependekezwa kuwa balozi mpya wa Marekani nchini China amesema, ana imani ya kuondoa tofauti kati ya China na Marekani kwa manufaa ya nchi hizo mbili na dunia kwa ujumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako