• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yazindua mfuko wa kukabiliana na masuala ya mazingira

    (GMT+08:00) 2017-02-03 18:26:22

    Serikali ya Tanzania imezindua Mfuko wa Taifa wa Kuhifadhi Mazingira unaolenga kukabiliana na masuala ya mazingira, yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameleta mtikisiko nchini humo.

    Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira nchini Tanzania January Makamba, amesema mfuko huo utalenga kuunga mkono mashirika na vitendo vinavyohusiana na uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha matatizo yanayokabili mazingira nchini humo yanapungua.

    Makamba ameongeza kuwa, masuala ya mazingira yanajadiliwa kwa kiasi kikubwa sehemu mbalimbali duniani, na ni muda mwafaka kwa Tanzania kuanzisha mfuko maalum unaolenga kufadhili masuala ya mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako