• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapambano yasimamishwa mashariki mwa Ukraine

    (GMT+08:00) 2017-02-06 09:12:35

    Ukraine imesimamisha mapambano katika eneo la mashariki, na wizara ya ulinzi na usalama ya nchi hiyo imeilaani Russia kwa kuiletea Ukraine matatizo kwa makusudi kwenye kazi ya kukarabati miundombinu.

    Habari zinasema kwa mujibu wa mapendekezo ya Shirika la Usalama na Ushirikiano la Ulaya OSCE, eneo la Donbass, mashariki mwa Ukraine lingesimamisha mapambano tangu jana, na kuanza tena kazi ya kukarabati miundombinu.

    Wizara ya ulinzi na usalama ya Ukraine imesema inaunga mkono mapendekezo ya kusimamisha vita, na Ukraine imewasilisha waraka wa kuahidi kuhakikisha usalama na ukarabati wa miundombinu. Wakati huo huo, wizara hiyo pia imeilaani Russia kwa kukwamisha kazi ya kukarabati miundombinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako