• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Refa Andre Marrier kuchezesha fainali ya Manchester United dhidi ya Southampton

    (GMT+08:00) 2017-02-07 09:52:08

    Refa Andre Marriner amethibitishwa kuwa ndie Refa wa Fainali ya Kombe la Ligi huko England, EFL CUP, kati ya Manchester United na Southampton ambayo itachezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Jumapili Februari 26.

    Refa Marriner, mwenye Miaka 46, atasaidiwa na Richard West na Stuart Burt wakati Kevin Friend akiwa Refa wa Akiba.

    Msimu huu, katika Mechi 24 alizochezesha, Refa Marriner ametoa Kadi za Njano 92 na Kadi Nyekundu 5.

    Mapema mwanzoni mwa Msimu huu, Marriner aliiminya Man United Penati ya wazi walipotoka Sare 1-1 na Arsenal Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako