• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti mpya yaonesha wakenya milioni 2.7 wanahitaji msaada wa chakula

    (GMT+08:00) 2017-02-07 10:08:38

    Idara ya kitaifa ya usimamizi wa maafa ya Kenya NDMA imesema, idadi ya wakenya wanaohitaji msaada wa chakula imeongezeka kutoka watu milioni 1.3 katika mwezi wa Agosti mwaka jana hadi milioni 2.7 katika mwezi wa Januari kutokana na ukame ulioanzia mwaka jana.

    Idara hiyo imesema wengi wa wanaohitaji msaada ni wazee, wagonjwa, kina mama na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

    Idara hiyo imesema idadi hiyo ni karibu asilimia 20 ya watu kwenye maeneo ya wafugaji, na asilimia 18 ya watu kwenye maeneo ya pembezoni ya wakulima.

    Kenya imekuwa inakabiliwa na ukame wa muda mrefu, ambao wataalamu wameonya kuwa utafanya hali ya usalama wa chakula kuwa mbaya, na hatua mwafaka zinapaswa kuchukuliwa ili kupunguza hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako