• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la kulinda wanyamapori Afrika Mashariki laadhimisha miaka 60 tangu lianzishwe

    (GMT+08:00) 2017-02-08 10:13:17

    Shirika la kuhifadhi wanyama pori la Afrika Mashariki EAWLS limeadhimisha miaka 60 tangu libuniwe. Wakati wa maadhimisho hayo yalioleta pamoja wadau kadhaa wa kulinda mazingira na wanyama pori, waziri wa mazingira nchini humo Judi Wakhungu aliishukuru China kwa hatua yake ya kupiga marufuku uuzaji wa pembe za ndovu.

    EAWLS ilianzishwa mwaka wa 1956 ikijumuisha mashirika ya kuhifadhi wanyama pori kutoka Tanzania, Kenya na Uganda .

    Majukumu yake yamekuwa ni kuhifadhi mazingira, raslimali asili, wanyama pori, utafiti na kuelimisha jamii.

    Mkurungezi mkuu wa shirika hilo Bwana Julius Kamau anasema ndani ya miaka hiyo 60 wamehakikisha fahari ya Afrika Mashariki ya kuwa kitovu cha utalii imedumishwa.

    "Kama haingekuwa juhudi za waanzilishi wa shirika hili wengi wetu hapa hatungefurahia kuwaona wanyama tulio nao. Hivyo tuna jukumu la kufanya lolote tuwezalo kulinda mazingira ili watoto wetu waweze kufurahia mahadhari na turathi kama sisi. Mwanzoni shirika hili lililenga kulinda wanyama pori hasa wale walio katika hatari ya kuangamia. Tunafanikisha juhudi zetu za kulinda wanyama kwa kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi wanyama kama vile Koran a Nakuru na kukuza taasisi "

    Hata hivyo ndani ya miaka hiyo sitini, kanda hii imekuwa ikipoteza wanyama wengi hasa ndovu na vifaru kutokana na shughuli za ujangili.

    Soko kubwa la pembe za ndovu na vifaru barani Asia linadaiwa kuathiri pakubwa juhudi za kuhifadhi wanyama hao huku nchi kama vile Uganda ikisalia bila kifaru hata mmoja.

    Takwimu zinaonyesha kwamba Afrika imekuwa ikipoteza ndovu 30,000 kila mwaka kutokana na shughuli za ujangili.

    Lakini sasa kuna afueni baada ya serikali ya China kutangaza kwamba itapiga marufuku biashara ya pembe za ndovu kwenye ardhi yake.

    Kwa nchi kama Kenya inayotegemea sana utalii kwa mapato yake ya kigeni hatua hiyo itasaidia pakubwa juhudi zake za uhifadhi wa mazingira na wanyama pori.

    Bi Judi Wakhungu waziri wa mazingira na mali asili anasema.

    China nayo kwa upande wake imeahidi kuendelea kushirikiana nan chi za Afrika katika kuhifadhi mazingira na mali asili.

    Balozi wa China nchini Kenya Liu Xianfa anasema wakati biashara kati ya pande zote mbili ikiendelea kuongezeka pia serikali zinashirikiana kulinda mazingira na wanyama pori.

    "Kulinda wanyama pori kunahitaji bidii na kujitolea. Kama rafiki wa kutegemewa na kuaminika, China itatilia mkazo zaidi uhifadhi wa wanyama pori kama sehemu ya ushirikiano kati yake na Afrika. Katika mkutano wa FOCAC mjini Johanesburg Afrika Kusini Rais Xi Jinping alitangaza mpango mpana wa maendeleo ya kuhifadhi mazingira ikiwa ni moja wa nguzo kumi muhimu za ushirikiano kati ya China na Afrika. Miongoni mwa mambo aliotangaza ni kuwezesha afrika kukumbatia maendeleo ya kiviwanda yasio chafua mazingira. China pia itasaidia Afrika kuanzisha miradi 100 ya kuzalisha kawi safi na kulinda wanyama pori."

    Takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya watu katika kanda ya afrika mashariki inaongezeka kwa asilimai 20 kila mwaka, wote wakihitaji chakula, makazi na maji vitu ambavyo vinatishia raslimali asili.

    Kwa kufahamu hilo, mashirika kama EAWLS yanachukua hatua za mapema kutafuta suluhu kabla majanga hayajafikia viwango vya hatari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako