• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya jumla ya watu itafikia bilioni 1.42 ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2017-02-08 18:08:28

    Hivi karibuni Kamati ya afya na uzazi wa mpango ya taifa imetangaza Mpango wa maendeleo ya uzazi wa mpango kati ya mwaka 2016 hadi 2020, ukisema ifikapo mwaka 2020, idadi ya jumla ya watu nchini China itafikia bilioni 1.42, huku wastani wa idadi ya watoto ya kila mama ukiongezeka na kufikia 1.8. Wataalamu wanaona kuwa mpango huo una muhimu mkubwa kwa China katika kukabiliana na changamoto zinazoletwa na idadi ya watu katika siku za baadae. --- ana maelezo zaidiā€¦

    Kwa mujibu wa mpango huo, ifikapo mwaka 2020 idadi ya jumla ya watu kote nchini itafikia bilioni 1.42, na kiwango cha ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka kitakuwa 6 ya elfu moja, hali inayomaanisha kuwa idadi ya watu itaweza kuongezeka kwa watu milioni 45 katika kipindi cha Mipango ya 13 ya miaka mitano.

    Kutokana na mpango huo, kati ya mwaka 2016 hadi 2020, kiwango cha jumla cha uzazi (Total fertility rate) kitakuwa 1.8. Kiwango hicho ni takwimu muhimu kwa utungaji wa sera kuhusu idadi ya watu, na kinaonesha wastani wa idadi ya watoto wa kila mama. Mkuu wa Chuo cha idadi ya watu katika Chuo Kikuu cha umma cha China ambaye pia ni mkurugenzi wa Taasisi ya idadi ya watu ya China Bw. Zhai Zhenwu anasema:

    "Kiwango cha juu cha uzazi kinamaanisha kuwa idadi ya jumla ya watu inazidi kuongezeka, na tofauti yake ni kuwa kiwango cha chini cha kinamaanisha idadi ya wazee inaongezeka kwa kasi zaidi. Kiwango cha cha 1.8 kinachowekwa kwenye Mpango wa idadi ya watu ni mwafaka, kwani inamaanisha kuwa idadi ya jumla ya watu itaongezeka kwa taratibu na itafikia kilele mwaka 2028, na baada ya hapo kupungua hatua kwa hatua. Wakati huo huo idadi ya wazee haitakuwa kwenye kiwango cha juu sana."

    Ili kuhakikisha ongezeko mwafaka la idadi ya watu, kazi kuu ya Mpango wa maendeleo ya uzazi wa mpango ni utekelezaji wa pande zote wa sera ya "watoto wawili". Mpango huo unasisitiza kuelekeza na kuhimiza nguvu ya jamii kuanzisha mashirika ya utoaji wa huduma zinazohusika zikiwemo hospitali zisiyo za biashara kwa wanawake na watoto, na shule za chekechea, pia unatoa mwito wa kuharakisha hatua ya kujenga zana za kuwahudumia watoto na watoto wachanga katika sehemu za umma na ofisini.

    Hivi sasa katika miji mikubwa, familia nyingi zina wasiwasi ya kuwa na mtoto wa pili kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo kutokuwa na mtunzaji wa mtoto na gharama kubwa za malezi. Akizungumzia suala hilo Bw. Zhai Zhenwu anaona kuwa inapaswa kuanzisha mashirika ya utunzaji wa watoto wadogo, ili kuondoa wasiwasi kwa wanawake hao wanaotaka kuwa na mtoto wa pili. Pia anaona kuwa katika miaka mitano ijayo, muundo wa idadi ya watu nchini China utabadilika kwa kiasi, anasema:

    "Naona kuwa katika miaka mitano ijayo mwendo wa ongezeko la idadi ya wazee utapungua. Hali hii inatokana na kuwa idadi ya watu waliozaliwa kuanzia mwaka 1958 hadi 1961 ni ndogo, hali ambayo itafanya idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 itakuwa chache itakapofika kati ya mwaka 2018 hadi 2021. Hali hii inaipatia China muda wa kuchukua hatua ili kukabiliana na suala linaloletwa na idadi kubwa ya wazee. Mbali na hayo kutokana na utekelezaji wa sera ya "watoto wawili", na maendeleo ya miji, uwiano wa idadi ya watoto wa kiume kwa watoto wa kike (Sex Ratio) kitazidi kupungua."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako