• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 20 ya ulinzi wa watoto kwenye maeneo yenye mapigano

    (GMT+08:00) 2017-02-09 09:17:57

    Umoja wa Mataifa umeadhimisha miaka 20 ya ulinzi wa watoto kwenye maeneo yenye mapigano, kwa viongozi wa juu wa Umoja huo wakipongeza miongo miwili ya juhudi za dunia katika kuwaokoa watoto kutokana na mateso ya vita.

    Akiwasilisha ujumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano uliofanyika katika makao makuu ya Umoja huo mjini New York, mkurugenzi wa ofisi ya katibu mkuu huyo Bibi Maria Luiza Viotti amesema, jukumu hilo limesaidia kuleta tofauti dhahiri kwenye maisha ya watoto wa nchi nyingi. Amesema kutokana na juhudi za pamoja za serikali mbalimbali, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kijamii, zaidi ya watoto laki 1.15 wameokolewa kutoka kwa makundi yenye silaha na majeshi ya nchi.

    Hata hivyo, Katibu mkuu huyo amesema, kuendelea kuwepo kwa migogoro kunawaweka watoto kwenye hatari kubwa, na njia pekee ya kuwalinda watoto hao ni kuzuia migogoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako