• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Allan Nyom asema hajutii kuikana Cameroon- AFCON 2017

    (GMT+08:00) 2017-02-09 09:31:35

    Beki wa West Brom, Allan Nyom amesema hajutii kukataa kwenda kuichezea Cameroon na kubaki na klabu yake, West Brom.

    Cameroon iliifunga Misri na kubeba taji la Kombe la Mataifa ya Afrika Nyom alikuwa miongoni mwa wachezaji kadhaa walikataa kwenda kuichezea nchi yao kwenye michuano hiyo nchini Gabon.

    Wengine ni pamoja na Joel Matip aliyeamua kubaki na Liverpool nchini England.

    Nyom amefika mbali zaidi na kusema kuwa hata kama kabla ya mashindano wangemuambia Cameroon inakwenda kutwaa Kombe na hayumo kikosini, asingejali kwa sababu anafuraha anachezea klabu, ambayo ni muhimu zaidi kwake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako