• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama kuu ya Kenya yaamua kuwa kufunga kambi ya Dadaab kunakiuka katiba

    (GMT+08:00) 2017-02-10 09:47:04

    Mahakama Kuu ya Kenya imetoa hukumu kuwa amri ya kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Kenya inakiuka katiba.

    Jaji John Matiwo wa mahakama hiyo amesema serikali imekiuka sheria, kwa kuwa hadi sasa katika kambi hiyo hakuna mkimbizi yeyote anayekutwa na hatia, na wala hakuna ushahidi wa kuwepo kwa wanachama wa Kundi la Al-Shabaab ndani ya kambi hiyo.

    Kabla ya hapo mashirika mawili ya haki za binadamu ya Kenya yanaona amri ya serikali ya Kenya kufunga kambi ya wakimbizi na kufunga ofisi inayoshughulikia mambo ya wakimbizi ni ukiukaji wa haki za binadamu. Kwa hiyo mashirika hayo yameiomba mahakama ifanye uchunguzi kuhusu uhalali wa amri hiyo ya serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako