• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump asema alikuwa na mazungumzo mazuri sana na rais Xi wa China

    (GMT+08:00) 2017-02-11 17:48:21

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema alikuwa na "mazungumzo mazuri sana" na mwenzake wa China Xi Jinping.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na waziri mkuu wa Japani Shinzo Abe katika Ikulu ya Marekani, rais Trump amesema yeye na rais Xi walijadili masuala mengi kwenye mazungumzo hayo marefu yaliyofanyika kwa njia ya simu. Amesema China na Marekani ziko kwenye "mchakato wa kupatana vizuri", hali ambayo ina manufaa kwa nchi zote kwenye eneo la Asia na Pasfiki ikiwemo Japani.

    Ikulu ya Marekani imesema Trump na Xi walifanya mazungumzo ya "dhati mno" kwa njia ya simu, ambapo Trump alikubali kuheshimu sera ya China moja, msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya China na Marekani katika miongo kadhaa iliyopita, ambayo inatambua serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali ya China

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako