• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 17 wafa kwa kukanyagana kaskazini mwa Angola

    (GMT+08:00) 2017-02-11 17:57:48

    Watu wasiopungua 17 wamefariki na makumi ya wengine wamejeruhiwa kwa kukanyagana jana usiku katika uwanja wa soka mjini Uige, kaskazini mwa Angola.

    Msiba huu ulitokea usiku wa Ijumaa au dakika saba baada ya kuanza kwa mechi ya soka ya ngazi ya A kati ya timu ya Santa Rita de Cassia na ile ya Libolo wakati mamia ya mashabiki wa soka walivunja moja ya milango ya uwanja huo ili kuangalia mechi hiyo

    Duru zinazopatikana na hospitali ya huko zinasema kumekuwa na wahanga 76, na kati yao 17 wakiwa wamefariki, ambao wengi wao ni vijana wasio na tiketi wakijaribu kujipenyeza kwa uwanja huo ili kuangalia mechi. Na watu watano wameripotiwa kuwa katika hali mbaya.

    Mashuhuda walisema watu hawa waliojaribu kuingia uwanjani wamezidi uwezo wa uwanja huo unaoweza kubeba watu elfu nane.

    Rais Jose Eduardo dos Santos wa Angola ameamuru uchunguzi kuhusu tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako