• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki za Kenya zalazimika kufunga matawi na kupunguza wafanyakazi kutokana na matumizi ya njia za kidigitali.

    (GMT+08:00) 2017-02-13 19:08:28

    Benki za Kenya zinafunga baadhi ya matawi yake na kupunguza wafanyakazi, kutokana na kufuata mkakati wa kutimiza njia za kutoa huduma kidigtali na kupunguza gharama za utendaji, baada ya serikali kuweka ukomo kwenye riba.

    Mwezi Septemba mwaka jana Benki Kuu ya Kenya iliweka ukomo wa riba ya asilimia 4 zaidi ya kiwango cha asilimia kumi ya sasa.

    Kutokana na hatua hiyo taasisi 10 za fedha kati ya 42 zinazotoa huduma nchini Kenya, zilitangaza kupunguza wafanyakazi zaidi ya 970 na kufunga matawi 21.

    Wachambuzi wanasema benki za Kenya kwa sasa hazina chaguo, ila kutoa huduma kwa njia za kidigitali, ili kukabiliana na mashirika ya mawasiliano ya habari yanayotoa huduma za fedha

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako