• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga Japan kuishawishi Marekani kuunga mkono matakwa yake haramu kuhusu ardhi

    (GMT+08:00) 2017-02-13 20:21:17

    Japan na Marekani hivi karibuni zilitoa taarifa ya pamoja zikisema "Mkataba wa ulinzi kati ya Marekani na Japan" unavihusisha visiwa cha Diaoyu. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, kisiwa cha Diaoyu na visiwa vilivyoko pembezoni mwake viko kwenye ardhi ya China tangu enzi na dahari, na China inapinga Japan kuishawishi Marekani kutoa ahadi za kuunga mkono madai yake yasiyo halali kwa jina la Mkataba huo.

    Kuhusu suala la bahari ya kusini ya China, msemaji huyo amesema China ina mamlaka isiyopingika kwenye visiwa mbalimbali vilivyo kwenye bahari ya kusini ya China na maeneo ya bahari yaliyo karibu. Ameongeza kuwa China kufanya ujenzi katika visiwa hivyo ni mamlaka yake, na sio kwa ajili ya malengo ya kijeshi.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, China inapinga Korea Kaskazini kukiuka azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kurusha kombora la masafa marefu na kutoa wito pande zote kujivumilia na kulinda amani na utulivu wa kanda hiyo kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako