• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani ajiuzulu kutokana na mawasiliano yenye utata na Russia

    (GMT+08:00) 2017-02-14 20:17:30

    Mshauri wa maswala ya usalama wa Marekani Bw Michael Flynn amejiuzulu siku kadhaa baada ya habari kuwa aliwasiliana kwa njia ya simu na mwanadiplomasia wa Russia, kuhusiana na vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Russia, kabla ya Rais Donald Trump kuapishwa kuwa rais wa Marekani.

    Kujiuzulu kwa Bw Flynn kunafuatia ripoti kuwa aliongopa kuhusu kujadili kwa njia isiyo sahihi vikwazo vya Marekani dhidi ya Russia na Balozi wa Russia nchini Marekani.

    Jana ilifahamika kuwa wizara ya sheria ya Marekani iliiarifu Ikulu ya Marekanai kuwa Bw Flynn hakuwa mkweli kuhusu mawasiliano yake na balozi wa Russia na anaweza kuwa na hatari ya kutumiwa na Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako