• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  PSG yaituliza Barcelona, Di Maria atupia mbili

    (GMT+08:00) 2017-02-15 08:29:47

    PSG imefanikiwa kuilaza Barcelona kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

    Barcelona ikiwa ugenini jijini Paris imeshindwa kuonyesha cheche licha ya kuongozwa na nyota wake Lionel Messi na Neymar na kujikuta ikipokea kipigo hicho cha kondoo mchovu.

    Angelo Di Maria ametumbukia nyavuni mara mbili huku Endson Cavani aliyetimiza miaka 30 jana akifunga moja na Julian Draxler akifunga moja.

    Mechi nyingine Benfica imeifunga Borussia Dortmund kwa bao 1-0. Leo michezo miwili itapigwa ambapo Bayern Munich itacheza na Arsenal, huku Real Madrid itakutana na Napoli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako