• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kukamtwa kwa mrithi wa Samsung kwaongeza uwezekano wa kurefushwa kwa uchunguzi kuhusu kashfa dhidi ya rais wa Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2017-02-17 19:24:11

    Mahakama ya Seoul nchini Korea Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa makamu mkuu wa kampuni ya vifaa vya umeme ya Korea Kusini Samsung Bw. Lee Jae Yong, na kuonyesha uwezekano wa kurefusha uchunguzi unaofanywa na waendesha mashtaka kuhusu kesi ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Rais Park Geun Hye.

    Tume huru inayofanya uchunguzi kuhusu kashfa hiyo inatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake kuhusu kashfa inayomkabili Rais Park mwishoni mwa mwezi huu, lakini kama Bw. Lee atakamatwa unaweza kurefushwa.

    Tume hiyo imeomba kurefushwa kwa muda wa uchunguzi, lakini inaonekana kuwa waziri mkuu wa Korea Kusini ambaye ni mshirika wa karibu Rais Park, atakakaa ombi hilo.

    Chama kikubwa cha upinzani kimewasilisha mswada wa kutaka uchunguzi wa kashafa hiyo uendelee, lakini chama tawala hakitaki uchunguzi huo uendelee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako