• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China asema uendelezaji wa uhusiano wa kiwenzi na Afrika unawanufaisha waafrika

    (GMT+08:00) 2017-02-18 18:55:57

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema, maendeleo ya uhusiano wa kiwenzi na Afrika yanategemea amani na hatua za kujiendeleza, pia yanahitaji kuchukua hatua za kuunga mkono na kuisaidia Afrika.

    Wang amesema hayo katika mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi 20 ulioanza jana huko Bonn, Ujerumani.

    Wang amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuhimiza amani barani Afrika, kutoa uhakikisho kwa maendeleo ya Afrika, kuhimiza msukumo wa ongezeko la uchumi barani Afrika, kutatua matatizo yanayokabili maisha ya wananchi, na kuonesha sifa za nchi mbalimbali ili kushirikiana kuchangia maendeleo ya Afrika.

    Habari nyingine zinasema, Bw. Wang Yi pia amehutubia Mkutano wa 53 usalama wa Munich, na kufafanua msimamo wa China wa kanuni ya kushikilia kufanya ushirikiano kwa pamoja na kuchangia amani na maendeleo duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako