• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaahidi kuimarisha uratibu na nchi za BRICS kwa ajili ya maandilizi ya mkutano wa kilele

    (GMT+08:00) 2017-02-20 10:14:53

    China itaimarisha uratibu na nchi wanachama wa BRICS, ikiwemo Afrika Kusini, kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za BRICS unaotarajiwa kufanyika Septemba mjini Xiamen, kusini mashariki mwa China.

    Kauli hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nje ya China Bw Wang Yi alipokutana na mwenzake wa Afrika Kusini Bibi Maite Nkoana-Mashabane mjini Beijing.

    Bw Wang amesema mkutano huo utasukuma mbele maendeleo ya pamoja ya nchi za BRICS, na kuhimiza mafungamano ya kiuchumi yaliyo shirikishi na yenye uwiano zaidi.

    Bibi Nkoana-Mashabane amesema China ni mwenzi muhimu wa kimkakati kwa Afrika Kusini, na Afrika Kusini iko tayari kuzidisha uaminifu wa kisiasa na wa kimkakati na China, na kuimarisha uratibu na China kwenye taratibu za ushirikiano wa kikanda na wa kimataifa, ikiwemo BRICS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako