• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kufanya maadhimisho ya miaka 18 ya Mpango wa bonde la mto Nile

    (GMT+08:00) 2017-02-21 09:52:23

    Tanzania inatarajiwa kufanya maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa Mpango wa bonde la mto Nile jijini Dar es Salaam.

    Maadhimisho hayo yatakayofanyika Februari 22 yatazikutanisha nchi 10 za Bonde la Mto Nile. Waziri wa Maji na umwagiliaji wa Tanzania Bw Gerson Lwenge amesema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka katika nchi zilizo kwenye bonde la mto huo yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan, Sudan Kusini na Misri.

    Amesema kwa zaidi ya miaka 10 Mpango wa Bonde la Mto Nile unafanya shughuli zinazolenga kusaidia nchi hizo kufikia malengo yao ya maendeleo kupitia ushirikiano na hadi sasa wameshakubaliana miradi 35 ya uwekezaji itakayosaidia upatikanaji wa chakula, maji na usalama wa nishati. Amesema kama miradi hiyo ikitekelezwa kikamilifu itanufaisha takriban watu milioni 30 hadi kufikia 2025.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako