• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia kuimarisha usalama kabla ya kuapishwa kwa rais mpya

    (GMT+08:00) 2017-02-22 19:53:33

    Serikali ya Somalia imeimarisha usalama mjini Mogadishu na sehemu za karibu, kabla ya rais mpya wa nchi hiyo Mohamed Abdullahi Mohamed kuapishwa leo.

    Waziri wa habari wa Somalia Mohamed Abdi Hayer amesema, serikali imetekeleza mipango mbalimbali ya kuhakikisha hafla ya kuapishwa kwa rais mpya inafanyika kwa amani.

    Hatua kali za usalama zimetekelezwa katika barabara kuu mjini Mogadishu na sehemu nyingine muhimu.

    Mamia ya wanajeshi, maofisa na askari wa usalama wanafanya doria barabarani na amri ya kutotoka nje kwa saa 24 mjini Mogadishu inatekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako