• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia mazungumzo ya amani ya Geneva kuhusu suala la Syria yatapata matokeo mapema

    (GMT+08:00) 2017-02-23 18:50:16

    Mjume maalumu wa China anayeshughulikia suala la Syria Bw. Xie Xiaoyan jana alikutana na mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Staffan de Mistura, na kubadilishana maoni kuhusu mchakato wa kisiasa wa suala la Syria na mazungumzo yatakayofanyika mjini Geneva.

    Bw. Xie Xiaoyan amesema, mazungumzo ya amani ya Geneva yanapaswa kufuata matakwa ya azimio namba 2254 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na kutatua masuala rahisi kwanza na baadaye magumu, ili kupata matokeo mapema.

    Bw. de Mistura amesema, kuanzisha tena mazungumzo ya Geneva ni hatua muhimu ya kutekeleza azimio la 2254, pande mbili za mgogoro wa Syria zinatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu usimamizi wa mpito, kutunga katiba na kufanya uchaguzi. Ameongeza kuwa, Umoja wa Mataifa unaipongeza China kwa kushika msimamo wa haki na kufanya juhudi katika suala la Syria.

    Habari nyingine zinasema, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, China inaunga mkono mazungumzo ya amani kuhusu suala la Syria yanayofanyika leo mjini Geneva, na kutumai pande mbalimbali husika zitaongeza uaminifu kupitia mazungumzo hayo, na kupata matokeo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako