• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jamie Vardy afanikiwa kuondoa ukame wake wa magoli uliodumu tangu Disemba

    (GMT+08:00) 2017-02-24 09:27:28

    Jamie Vardy amefanikiwa kuondoa ukame wake wa mabao uliodumu tangu Desemba kwa kuifunga Sevilla na kuweka hai matumaini ya klabu hiyo katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

    Vardy amecheza mechi tisa bila kufunga tangu alipofunga mabao matatu dhidi ya Manchester City tarehe 10 Desemba. Lakini aliibuka tena na kufunga kutokana na krosi ya Danny Drinkwater zikiwa zimesalia dakika 17 ugenini Hispania na kuwapa bao muhimu la ugenini ingawa walilazwa 2-1.

    Awali Sevilla waliongoza 2-0 kutokana na mabao ya Pablo Sarabia na Joaquin Correa. Kipa wa Leicester Kasper Schmeichel pia aliwafaa sana kwa kuokoa mkwaju wa penalti kutoka kwa Correa. Mechi ya marudiano itachezwa uwanja wa King Power tarehe 14 Machi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako