• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya Chai kwenye soko la mnada Mombasa yateremka

    (GMT+08:00) 2017-02-24 18:12:13

    Bei ya Chai imeremka kwa shilingi 16 kwa kilo katika soko la mnada mjini Mombasa wiki hii ikiwa ni chini ikilinganishwa na wiki iliyopita. Kwa mujibu wa ripoti ya mamlaka ya chai nchini Kenya, wiki iliyopita bei ya Chai iliteremka hadi shilingi 305 kwa kilo hadi 286 kwa kilo jumanne wiki hii. Hii ni mara ya pili kwa bei ya chai kuteremka mwaka huu.Chama cha wafanya biashara wa chai Afrika mashariki kimesema kwa ujumla bidhaa hiyo ilikuwa chache katika soko la mnada mjini Mombasa ikilinganishwa na kipindi kilichopita.Mamlaka hiyo imeongeza kuwa upungufu wa zao hilo umetokana na ukame ambo umeendelea kushuhudiwa kote nchini Kenya.Wachambuzi wa soko la chai wamesema ukame ulioko hivi sasa utapunguza uzalishaji wa zao hilo kwa asilimia 12. Kenya ndio nchi inayoongoza katika uuzaji wa zao la chai kote duniani ambapo inauza asilimia 95 ya chai yake katika soko la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako