• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lapambana na kuwaua wapiganaji wa kundi la M23

    (GMT+08:00) 2017-02-24 20:54:15

    Waasi wa M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaripotiwa kusambazwa na jeshi la serkali ya nchi hiyo kupitia mapambano makali yaliyoshuhudiwa wiki hii maeneo ya MATEMBE na KIRINGA wilayani RUTSHURU, mkoani KIVU YA KASKAZINI.

    Kwa mujibu wa jeshi la serkali, waasi 16 waliuwawa na wengine watano wametekwa nyara; na 58 kujiripoti kwa vikosi vya serkali.

    Katika mapambano hayo makali yaliyoshuhudiwa mapema wiki hii bahina ya vikosi vya serkali na wa waasi hao wa M23 mashariki mwa jamahuri ya kidemokrasia ya Congo na ambayo hadi alhamisi ilikuwa vigumu kutoa matukio kamili ya mapambano yenyewe;atimaye jeshi la taifa kupitia msemaji wa opersheni zinazowasaka waasi hao pamoja na makundi mengine yanayoshikilia silaha kinyume na sharia za nchi;liliiambia idhaa hii ya Kiswahili ya kwamba;waasi walipata pigo kubwa;wakiwapoteza wapiganaji wao waliyoanguka kwenye uwanja wa mapambano;wengine wao kutekwa nyara;na idadi kubwa kujiripoti.

    Ili kupata ufafanuzi zaidi;Msemaji huyo wa kijishi meja NDJIKE KAUKO GUILAUME,aliye msemaji wa operesheni SOKOLA 2 inayomaanisha safisha ya pili katika lugha la kiswahili;kwa njia ya simu alitupa matukio haya:

    "Matukio ya mapambano na hao waasi ni kwamba wapiganaji wao 16 waliuwawa, 5 walitekwa nyara; 58 walijiripoti kwa vikosi vya serkali,bila ya kusahahu silaha tulizokamata"

    Nilijaribu vilevile kumtafuta kwa njia ya simu kiongozi wa M23 apatikanaye mjini KAMPALA/Uganda Bw BERTRAND BISIMWA,kwa ajili ya kupata duru lao;juudi zetu,ziligonga mwamba.

    Hata hivyo wasiwasi ni mwingi miongoni mwa raia wa kawaida,wanaohofia huenda;kurejea upya kwa kundi la M23;kukahathiri maisha yao ya kawaida;haswa wengi wakiwa na wasiwasi wa kuzorotesha mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu kama wanavyosimulia hapa Mmoja wao amesema,

    "Tunajiuliza;kwa nini watu wako wakitarajia kufanya uchaguzi;tena wanapenda kukuja kutusumbuwa;au ni unjanja wa wanasiasa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako